
Nyaraka za Tweve Partner
Nani anaweza kuwa partner?
Mtu yeyote mwenye namba ya simu ya Tanzania na uwezo wa kutangaza mtandaoni. Hauhitaji mtaji, hauhitaji ujuzi wa kiufundi — unachohitaji ni kusambaza link yako kwa marafiki, familia na wafuasi wako kwenye mitandao ya kijamii. Pata kipato bila kufanya kazi ngumu.
Tweve Partner ni nini?
Ni programu ya washirika (affiliate) ya Tweve Max. Kama partner, unatangaza Tweve Max kwa kutumia link yako ya kipekee ya referral. Kila mtumiaji anayefungua akaunti na kununua kifurushi kupitia link yako, unapata sehemu ya faida.
Ninawezaje kuwa partner?
Fungua akaunti bila malipo kwa namba yako ya simu na nenosiri. Baada ya kujisajili, utapewa referral link yako mara moja — hakuna gharama, hakuna masharti magumu.
Ninapata pesa kiasi gani?
Kwa chaguo-msingi, unapata 50% ya faida ya kila kifurushi kinachonunuliwa kupitia link yako. Asilimia hii inaweza kubadilishwa na Tweve Max. Kumbuka: mgawo hutokea PALE TU mtumiaji ananunua kifurushi (package) — sio kwa michezo, sarafu au vitu vingine.
Ninatoaje pesa zangu?
Kutoka dashboard yako, bonyeza "Toa Pesa" (Withdraw), weka kiasi na namba ya simu ya kupokelea. Ada ndogo ya 2% hukatwa kwenye kiasi unachotoa. Tweve Max itakutumia pesa moja kwa moja kwenye simu yako.
Kuna masharti ya kutoa pesa mara ya kwanza?
Ndio. Ili kutoa pesa mara ya kwanza, lazima uwe umepata angalau TZS 10,000 na uwe na angalau watumiaji 15 walioingia kupitia link yako. Baada ya hapo, unaweza kutoa wakati wowote. (Viwango hivi vinaweza kubadilishwa na Tweve Max.)
Naweza kufanya nini kingine na salio langu?
Unaweza kuhamisha pesa kwa partner mwingine kwa kutumia code au namba yao. Pia unaweza kutumia salio lako kununua kifurushi cha Tweve Max kwa namba yoyote ya simu unayochagua.
Naona nini kuhusu watumiaji wangu?
Dashboard yako inakuonyesha watumiaji wote walioingia kupitia link yako — wangapi wako hai (wana kifurushi) na wangapi hawajanunua bado. Hii inakusaidia kufuatilia mafanikio yako.